Muuzaji Za Pembejeo Ya Kilimo

Pembejeo (input) ya kilimo ni kifaa chochote cha nje ambayo inaweza kuwekwa kwa udongo, inaweza kusaidia mimea za mkulima kukua vizuri. Zinaweza kukuwa vitu vyovyote kama mbegu ya kiwango/hali cha juu, trekta ya teknolojia ya juu. Zimegawanywa kwa vikundi viwili kama pembejeo (inputs) za kuliwa (consumables input) na pembejeo (inputs) za mitaji (capital goods). Pembejeo ya kuliwa ni bidhaa za kutumia kila siku kwa kilimo cha wakulima wadogo kama mbegu za hali za juu, mbolea (fertilizer) dawa ya kuua wadudu (insecticides and pesticides), majani (straws), nyasi (hay), mtego wa madudu, maji na kadhalika. Pembejeo ya mtaji (capital inputs), ni pembejeo ya kilimo ambayo ni ya kimakanika na ya teknolojia ya juu kama Chandarua cha nailoni (Nylon netting), vigingi ( stakes), majembe (plows), mfumo wa kunyunyuzia, na nyenzo za trellising(trellising materials).

Add to Bookmarks
Print Friendly, PDF & Email
(Visited 120 times, 1 visits today)

Wauzaji wa pembejeo za kilimo kwa idadi ndogo, ni bidhaa huru za kusambazwa ya pembejeo ya kilimo, kama madawa ya kuua madudu (pesticides). Muuzaji wa kilimo ni mwenye biashara ambaye anauza, anasambaza bidhaa za kilimo kama mbegu, mbolea (fertilizers), suluhiso za akiba (stock remedies), kemikali za kilimo, chakula cha wanyama na huduma zingine ambazo zinafaa kukuwa karibu na wakulima.

Muuzaji wa pembejeo ya kilimo ana jukumu la kuleta pembejeo za kilimo  na pembejeo ambazo zinahusiana na kilimo karibu na wakulima, msimu bora na kutoa ushauri wa kilimo bora kwa wakulima, kilimo cha kupanda mimea mbalimbali pomoja, usimamizi jumuishi la wadudu (integrated pest management), kutunza/kuchunga na kulisha ngombe, na aina mbalimbali wa ufugaji.

Wakulima wote Uganda ambao wanapokea mapato kutoka kwa kilimo na ufugaji wanafaa kusajiliwa na;

– Ofisi ya Huduma ya Usajili Uganda (URSB) kwa Cheti cha Kusajili Kuingiza  Kampuni / Shirika (incorporation) au Cheti cha Usajili wa mtu binafsi.

– Shirika ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) kwa kodi.

Tafadhali jua:

Kama mkulima amesajiliwa anahitajika kutii/kuhesimu sheria ya Mashrika za statutari kama

– Wizara wa Kilimo, Viwanda vya Wanyama na Uvuvi

– Shirikisho (Federations) ya Kitaifa cha Wakulima Uganda (UNFFE)

Kwa mtu binafsi

– Kitambulisho cha Kitaifa (ID)

– Cheti cha Kusajiliwa

Kwa mtu asiye binafsi/kampumi  (non individual )

– Fomu ya Kampuni 20

– Cheti cha kusajiliwa/kuingiza Kampuni/Shirika

Bonyeza/finya hapa ili upokee habari zaidi za kusajiliwa

– Unafaa kutembelea tovuti ya URA kwa www.ura.go.ug

– Bonyeza/finya hapa ili ujisajili kwa kodi kama mtu binafsi

Bonyeza/finya hapa ili ujisajili kama mtu asiye binafsi  (non individuals) 

Wewe kama mlipakodi unahaki wa kusajiliwa kama mlipakodi, kwa usawa kuna wajibu wa kodi ambazo unafaa kutimiza (fulfill) kama mlipakodi.

Bonyeza/finya hapa ili upokee habari kuhusu haki na wajibu wako kama mlipakodi ?

Unafaa kuweka rekodi za shughuli za biashara zote. Ni muhimu kama unaweka rekodi ambazo ziko na tarehe za shughuli za biashara ili kutambua kila ripoti na muda yake na hizi ni;

  • Rekodi ya stetimenti/habari ya mapato
  • Rekodi ya risiti na ankara (invoice)
  • Vocha za malipo
  • Ratiba za uagizaji (imports) kama wewe ni muagizaji
  • Mkataba ambazo zimefanywa/zimetimizwa
  • Stetimenti/habari za benki
  • Barua za kuajiri wafanyakazi na ushahidi ya malipo ya msahara.
  • Gharama/bili ya malipo ya vitu vya matumizi kama umeme/maji
  • Rekodi za bidhaa
  • Watu ambao biashara inawadai na Wenye wanadai biashara (Debtors and Creditors)

–  Weka rekodi zote za shughuli za biashara vizuri kwa lugha ya Kizungu

– Kama unataka kuweka rekodi kwa lugha ingine, tuma maombi kwa maandishi na sababu sahihi kwa Kamishna.

– Kama rekodi haiko kwa Kizungu, utahitajika kulipa gharama ya kutafsiriwa  (translation) kutoka kwa mtu wa kutafsiri ambaye amethibitishwa na Kamishna.

– Weka rekodi vizuri ili utambuaji wa kodi ambazo zinafaa kulipwa inarahisishwa

– Weka rekodi kwa miaka mitano baada ya wakati wa kodi kupita, ambayo inahusika na kodi ili itatumika kwa kumbukumbu (reference) mbeleni

– Unafaa kuchunga/kuweka rekodi ya biashara kwa miaka mitano wakati wowote.

– Rekodi ambazo zimewekwa zinafaa kukuwa za shughuli za biashara kwa kina na inafaa kuwekwa kwa njia ambayo itakuwa rahisi kulipata ikihitajika na kugeuzwa kwa aina ambayo inaelewekwa kwa urahisi.

Mtu yeyote ambaye anashughulika kwa biashara ya kilimo anahitajika kujisajili kwa kodi ya mapato. Kodi ya mapato inafaa kulipwa na aina za watu wote ambao wanapokea mapato kama mtu binafsi (individual), mtu asiye binafsi (non individual ) na ushirikiano (partnership )

Kodi ya kampuni/shirika (corporation tax)

Kodi hii inawekwa kwa makampuni zote Uganda kwa kiwango/cheo cha 30%. Mwenye biashara/muuzaji ya pembejeo ya kilimo  (agri input) lazima asajiliwe kwa kodi hii kama anafanya/shughuli kama Kampuni.

Kodi ya mapato

Hii ni kodi ambayo inawekwa kwa mtu binafsi kwa sekta na cheo cha mtu binafsi inatumika.

Bonyeza/finya hapa ili upokee habari kuhusu kodi ya mapato.

Lipa Ukiingiza Mapato (PAYE)

Kwa sekta hii inalipwa na wafanyakazi wanaopokea zaidi ya Shilingi 235,000 kila mwezi. Mwajiri anabakisha halafu anapereka/anawasilisha kwa URA.

Bonyeza/hapa ili upokee vyeo  vya PAYE

Kodi ya kubakisha (WHT)

Italipwa na muuzaji wa pembejeo ya kilimo  (agri input ) akisambaza bidhaa kwa ajenti aliyethibitishwa kubakisha kodi (witholding agent) kama thamani ya ankara (invoice value) inazidi Shilingi 1,000,000 ya Uganda.

Ninawezaje kurejesha retani kama muuzaji wa pembejeo ya kilimo (agri input) ?

Bonyeza/finya hapa ili upokee habari kwa namna ya kurejesha retani.

 

Baada ya kurejesha retani unafaa kulipa kodi ukitumia jukwaa zifuatazo kama benki, pesa kwa simu rununu, VISA, Mastakadi nakadhalika.

Tafadhali jua:

Tarehe kamili ya kurejesha retani ni sawa na tarehe kamili ya malipo.

Bonyeza/finya hapa ili usajili malipo

Uandishi/maelezo

Motisha ya kodi (Tax incetives)

Kinyunyuzi cha kilimo  (agricultural sprayer )

● VAT inasamehewa kama imeletwa nchini na muuzaji chini cha sheria ya VAT

 

●Kusamehewa kodi zote kama zimeletwa nchini na muuzaji wa shughuli ya kilimo chini cha Ratiba ya 5 ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004.

Kemikali ya Kilimo  (dawa ya kuua wadudu na dawa ya kuvu) (fungicides and pesticides)

● VAT inasamehewa kama zimeletwa nchini na muuzaji chini cha Sheria ya VAT.

 

● Kusamehewa kodi zote kama zimeletwa nchini na muuzaji wa shughuli ya kilimo chini cha Ratiba ya 5 ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004.

Vyombo/ufungani vya upakiaji ambazo zimeundwa za kupakia bidhaa za kusafirisha nje ya nchi.

Kusamehewa kodi zote kama zimeagizwa na nia ya kutumia kwa kupakia bidhaa za kusafirisha nje ya nchi, 2004.

Jembe ya kulima (ploughs),  Harowi (Harrows),  mbegu (seeders), wapandaji na wapandikizaji ( planters and transplant), kifaa cha kusambaza mbolea (fertilizer) na samadi (manure)

 

● VAT inasamehewa kama imeletwa nchini na muuzaji chini cha sheria ya VAT.

 

Kusamehewa kodi zote kama zimeletwa nchini na muuzaji wa shughuli ya kilimo chini cha Ratiba ya 5 ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004.

 

Mbolea (Fertilizers)

Mboplea ni nyenzo (material) asili (natural) au chanzo cha sintetiki (ambayo sio ya nyenzo ya chokaa (liming), ambayo inawekwa kwa udongo au kwa mimea, mara nyingi ni matawi ambayo inasambaza virubutisho (nutrients)  kutoka kwa mimea moja au zaidi ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa mimea

● Kusamehewa kodi zote chini cha Ratiba ya 5 ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004 kama imepitishwa na Wizara wa Kilimo Viwanda vya Wanyama na Uvuvi (Fisheries)

Mbegu ya kupanda, spora (spores) na mimea ambazo zimekatwa.

 

Mbegu ni mimea ya kiinitete (embryonic)  ambayo imefunikwa na ngozi ya nje

● Kusamehewa kodi zote chini cha Ratiba ya 5 ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004.

 

 kama imepitishwa na Wizara wa Kilimo Viwanda vya Wanyama na Uvuvi (Fisheries).

Kemikali ya kutumia kwa wanyama (vertinary acaricides)

● VAT inasamehewa kama zimeletwa nchini na muuzaji chini cha Sheria ya VAT.

 

● Kusamehewa kodi zote kama zimeagizwa na mwenye shughuli ya kilimo chini cha Ratiba ya 5 ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004.

Vyakula/malishe vya mifugo

● VAT inasamehewa kama zimeagizwa na muuzaji chini cha Sheria ya VAT.

 

● Kusamehewa kodi zote kama zimeagizwa na muuzaji wa shughuli ya kilimo chini cha Ratiba ya 5 ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, 2004

 

Ukitaka usaidizi zaidi, tembelea ofisi yetu ya URA iliyo karibu ili upokee usaidizi au piga simu  bila malipo 0800117000/0800217000 au WhatsApp: 0772140000

Add to Bookmarks (0)
Skip to content