Usindikiaji wa samaki ni nini?
Usindikiaji wa samaki inajumuisha shughuli ambazo zinaongeza thamani kwa samaki ya kuwashilisha/kuchukua kwa wateja.
Hapa Uganda hizi zinafanywa na makampuni za kufanya usindikiaji wa kusambaza kwa hoteli za viwango vya juu na kusafirisha nje.
Makampuni za kufanya usindikiaji wa samaki zote Uganda zinafaa kusajiliwa kwa kodi;
– Ofisi ya Huduma ya Usajili Uganda (URSB) kwa kampuni au jina la biashara
– Shirika ya Mamlaka ya Mapato Uganda kwa kodi
Tafadhali jua:
Kama umesajiliwa, unafaa kufuatilia marshati ya mashirika za kisheria kama;
Mtu binafsi (for individual )
– Kitambulisho I’D
– Cheti cha Kusajiliwa
Mtu asiye binafsi (for non individual)
– Fomu ya Kampuni 20
– Cheti cha Kusajili kampuni
Bonyeza hapa ili upokee habari kwa kina kuhusu mahitaji ya kusajili biashara ya usindikiaji wa samaki.
Unafaa kutembelea tovuti ya URA kwa www.ura.go.ug
– Bonyeza hapa ili usajiliwe kama mtu binafsi (for individual)
– Bonyeza hapa ili usajiliwe kama mtu asiye binafsi /kampuni (for non individual)
Bonyeza hapa ili upokee haki na wajibu wako kama mlipakodi
Kodi ya Shirika/kampuni (corporation tax)
Ni kodi ambayo inawekwa kwa wahusika kampuni/asiye mtu binafsi kwa cheo cha kawaida cha 30%.
Kodi ya mapato kwa mtu binafsi
Hii ni kodi ambayo inawekwa kwa mtu binafsi kwa sekta kwa cheo ambayo inafaa.
Bonyeza hapa kwa habari zaidi kuhusu cheo cha kodi cha mtu binafsi
Lipa Ukiingiza Mapato (PAYE)
Hii ni kodi kwa mhusika kwa sekta ambaye ako na wafanyakazi wa (utawala au wa kulipwa kwa kila siku) ambao wanapokea jumla ya mapato ambayo inazidi 235,000 kwa kila mwezi. Aina hii ya kodi inabakishwa kwa kila mwezi.
Bonyeza hapa ili upokee vyeo vya PAYE
Samaki ambazo zimefanyiwa usindikiaji imeongezwa thamani  VAT inatozwa kwa mauzo ya bidhaa kwa cheo cha kawaida ya 18%.
Kama samaki ambayo imefanyiwa usindikiaji inasafirishwa nje VAT inatozwa kwa cheo cha sifuri (0%).
Tafadhali jua:
Kampuni/mashine ya kufanya usindikiaji wa samaki lazima inafaa kusajiliwa kwa VAT na wanapaswaa kusajiliwa kwa EFRIS
Bonyeza hapa kwa habari zaidi kwa namna ya kusajiliwa kwa EFRIS
Kodi ya kubakisha (WHT)
Kodi ya kubakisha (WHT) ni kodi kwa mapato ambayo inabakishwa kwa chanzo na mtu mmoja (ajenti wa kubakisha ) kama amefanya malipo kwa mtu mwingine (payee). Kama Kampuni ya kufanya usindikiaji wa samaki imesambaza samaki juu ya milioni 1, mtu ambaye bidhaa imesambazwa kwake anafaa kutoza kodi ya kubakisha kwa cheo cha 6%. Kampuni inapokea Cheti cha Krediti ya Kodi (TCC) ambayo itawezesha ku-ofseti/kumaliza deni la kodi kwa wakati wa kurejesha retani ya mwisho wa kodi.
Bonyeza hapa kwa habari kuhusu kodi ya kubakisha.
Retani hii inajazwa namna ya retani zingine
Bonyeza hapa kwa habari zaidi kuhusu namna ya kurejesha retani ya kodi.
Â
Baada ya kurejesha retani, unahitajika kulipa kodi ambayo inafaa kwa kutumia jukwaa kama benki, simu rununu, VISA, Mastakadi, EFT, RTGs, msimbo wa USSD (*285#) nakadhalika.
Tafadhali jua;
Tarehe halisi ya kulipa kodi ni sawa na tarehe ya kurejesha retani.
Maelezo |
Motisha ya kodi |
Malori za friji |
Msamaha wa kodi zote chini cha ratiba ya 5 ya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2004. |
Nyumba baridi
Nyumba baridi ambazo mazingira baridi inadhibitiwa (namna friji inafanya kazi) |
Kodi ya uagizaji (import duty 0%) kulingana na EAC-CET inatoa usaidizi kwa kuweka mavuno na kutunza bidhaa za kilimo kwa mazingira baridi kama nyama ya ng’ombe, samaki, nyama ya kuku nakadhalika |
Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea ofisi ya URA ambayo iko karibu ili upokee usaidizi au piga simu kwa nambari ya bila malipo 0800117000/0800217000 au WhatsApp 0772141000