Bidhaa za samaki ya kusafirisha/mauzo ya nje

KAMPUNI YA KUSAFIRISHA SAMAKI NJE YA NCHI

Kusafirisha samaki nje ya nchi, ni harakati ambayo serikali inaruhusu makampuni na wanabiashara wadogo kuuza bidhaa zao kimataifa.

Bidhaa za samaki za kusafirisha nje inajumuisha samaki safi ambayo haijapozwa (fresh not chilled) waliopozwa na kuhifadhiwa (chilled and frozen fish) kaavu ambayo imechomwa (smoked), mizizi ya samaki (fish maws), chakula cha samakil, mafuta ya samaki, ngozi ya samaki na mapambo (ornamental). fileti ya samaki ni bidhaa za samaki ambazo zinasafirishwa kwa ukubwa kutoka Uganda kwa 76% ya uwingi na 78% ya jumla la thamani.

Add to Bookmarks
Print Friendly, PDF & Email
(Visited 15 times, 1 visits today)

Kodi ya Shirika/Kampuni (Corporation tax)

Ni kodi ambayo inawekwa kwa mtu asiye binafsi/kampuni kwa sekta hii kwa cheo cha kawaida cha 30%.

Kodi ya mapato ya mtu binafsi (Individual income tax)

Hii ni kodi ambayo inawekwa kwa mtu binafsi kwa sekta hii kwa kutumia cheo cha mtu binafsi ambazo zinafaa.

Bonyeza hapa ili upokee habari zaidi kuhusu cheo cha kodi ya mapato ya mtu binafsi.

Lipa Ukiingiza Mapato (PAYE)

Kodi hii inakuwa kwa wanaofanya shughuli kwa sekta hii ambao wako na wafanyakazi wa (Utawala na wale wa kupokea malipo ya kila siku) ambao wanapokea jumla la malipo ambayo inazidi 235,000/= kwa kila mwezi. Aina hii ya kodi inabakishwa kila mwezi.

Bonyeza hapa ili upokee vyeo vya (PAYE)

Wanaohusika kwa sekta ya samaki  wanafaa kusajiliwa na;

 • Ofisi ya Huduma ya Usajili Uganda (URSB) kwa Kampuni na jina la biashara
 • Shirika ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) kwa kodi

Tafadha jua:

Kama umesajiliwa unahitajika kufuatilia maasharti ya Shirika za kisheria kama;

 • Shirika ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA)
 • Idara ya Kudhibiti Uvuvi, Masharti na Kuhakikisha Kiwango kizuri cha Huduma chini cha Wizara wa Kilimo, Viwanda vya Wanyama na Uvuvi
 • Kwa wavuvi na wauzaji wa samaki, leseni lako haliwezi kurudishwa upya isipokuwa kama una TIN

Mtu binafsi (for individual)

 • Kitambulisho ID
 • Cheti cha Kusajiliwa

Kwa mtu asiye binafsi/kampuni (For non individuals )

 • Fomu 20 ya Kampuni
 • Cheti cha kusajili Kampuni

Bonyeza hapa ili upokee habari zaidi kuhusu mahitaji ya kusajili biashara yako ya uvuvi.

Unafaa kutembelea tovuti ya URA kwa www.ura.go.ug

 • Bonyeza hapa ili usajiliwe kama mtu binafsi
 • Bonyeza hapa ili usajiliwe kama mtu asiye binafsi/kampuni (non individual )

Unafaa kuweka rekodi ambazo zinahusiana na shughuli za biashara zako. Ni muhimu kukuwa na rekodi ambazo ziko na tarehe hii itakuwezesha kujua muda wa ripoti au wakati wa ripoti

 • Rekodi ya taarifa ya mapato
 • Rekodi ya risiti /Ankara (invoices)
 • Mizania (balance sheet)
 • Orodha ya malipo ya wanyakazi (payroll) na mkataba/barua ya kuajiriwa
 • Ratiba ya uagizaji (import schedules) kama iko
 • Taarifa/habari ya benki
 • Bili ya Matumizi kama ya (umeme au maji)
 • Rekodi ya stoki ya samaki
 • Rejesta ya mali (Asset register)
 • Watu wanaodai biashara na wenye biashara inawadai (debtors and creditors).
 • Mkataba wa usambazaji na malipo (contracts of supply)
 • Ratiba ya uagiza wa bidhaa na huduma (import schedules)

Weka rekodi vizuri vya shughuli za biashara zote kwa lugha ya kingereza.

–  Kama unataka kuweka rekodi kwa lugha tafauti,sarafu tuma maombi kwa maandiko ukiweka sababu sahihi kwa Kamishna ukiomba ruhusa.

Kama rekodi haijawekwa kwa lugha ya kingereza, utahitajika kugharamia kutafsiri (translations) kwa lugha ya kingereza na mtafsiri  ambaye amethibitishwa na Kamishna.

– Weka rekodi ili irahisishe uamuaji wa kodi yako;

– Weka rekodi kwa miaka mitano baada ya muda wa kodi kukamilika ambayo inahusika ili mbeleni kama kuna mahitaji ya kukagua vitabu au hati itakuwa rahisi

– Kama rekodi inahitajika kwa shughuli ambayo ilianza kabla ya miaka mitano kukamilika, utahitajika kuweka rekodi mpaka shughuli kukamilika

– Rekodi ambayo imewekwa inafaa kukuwa na ushahidi ambayo inatosha za taarifa/ habari za biashara na inafaa kuwekwa kwa umbizo/fomati ambayo itakuwa rahisi kubadilishwa kwa namna ya kawaida (standard form) ambayo itakuwa rahisi kueleweka.

Maelezo

Motisha ya Kodi

Malori za friji

Kusahemewa kodi zote chini cha ratiba ya 5 ya Shirika ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2004.

Nyumba baridi

Nyumba baridi ambayo ina halijoto (temperature) ambayo mazingira yake inadhibitiwa kama ya friji

Kodi ya uagizaji ni 0% kulingana na EAC CET inasadia kwa kudhibiti mavuno na uwekaji wa bidhaa za kilimo kwa nyumba baridi kama nyama ya ngombe, nyama ya kuku na samaki nakadhalika

 

 

Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea ofisi ya URA ili upokee usaidizi au piga simu kwa nambari ya bila malipo ya 0800117000/0800217000 au WhatsApp: 0772140000

 

Add to Bookmarks (0)
Print Friendly, PDF & Email
Skip to content