Studio za uzalishaji

Studio za uzalishaji ni nini?

Kampuni ya uzalishaji, nyumba ya uzalishaji, studio ya uzalishaji, ni kampuni au studio ambazo zinafanya  kazi kwa uwanja wa utendaji/kuigiza (performing) wa wasanii, vyombo vya habari vipya (new media art), filamu, redio, vichekesho (comics), Sanaa ya maingiliano (interactive arts), michezo za video, tovuti,muziki na video.

Wanahusika wa biashara ya uzalishaji wa maudhui (contents), au bidhaa kwa umbizo/fomati mbali mbali ikijumiisha tv na biashara ya redio, sauti ya muziki na video, filamu, programu ya televisheni, programu ya redio nakadhalika.

Add to Bookmarks
Print Friendly, PDF & Email
(Visited 7 times, 1 visits today)

Unahitajika kusajiliwa na;

  • Ofisi ya Huduma ya Usajili Uganda (URSB) kwa kusajili Kampuni.
  • Shirika ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) kwa kodi
  • Mamlaka ya Halmashauri ya Mtaa kama KCCA, Halmashauri ya Manispaa, kwa leseni ya biashara.

Tafadhali jua:

Kama umesajili, biashara utahitajika kufuatilia mahitaji za mashirika za kisheria kama;

  • Tume ya Mawasiliana Uganda (UCC).
  • Wizara ya Mawasiliano na Mwongozo wa Kitaifa.
  • Wizara ya Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii.

Kwa mtu binafsi (for individual)

  • Kitambulisho cha Kitaifa au kwa mawili zifuatazo, hati ya kisasa ya kukutambua, Pasipoti, Kadi ya kupiga kura, Kitambulisho cha kijiji, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha wakimbizi (refugee), Taarifa ya benki ya kisasa, Kibali cha kazi, Kadi ya fedha, Visa na Kadi ya NSSF nakadhalika.
  • Cheti cha Kusajiliwa (kama unabiashara)
  • Taarifa/maelezo ya kuhusu hati (deed) ya ushirikiano kama ni ushirikiano (partnership)

Kwa mtu asiye binafsi  (for non individual)

  • Fomu ya kampuni 20
  • Cheti cha kusajili Kampuni

Bonyeza hapa ili upokee mahitaji ya kuhusu kusajiliwa

Unafaa kutembelea tovuti ya URA kwa www.ura.go.ug

  • Bonyeza hapa ili ujisajili kama mtu binafsi (for individual)
  • Bonyeza hapa ili usajiliwe kama mtu asiye binafsi/kampuni

Bonyeza hapa ili upokee haki yako kama mlipakodi

Bonyeza hapa ili upokee wajibu wako kama mlipakodi

Kodi ambazo makampuni za uzalishaji /biashara za studio wanafaa kulipa ni hizi;

Kodi ya mapato – kwa watu wote, mtu binafsi na asiye binafsi ambao wanahusika.

Tafadhali jua:

Cheo ambacho kinafaa cha kodi ya mapato kwa kampuni/mtu asiye binafsi ni 30% kwa mapato ya taasisi ambacho kinafaa kutozwa (mapato ya jumla wakipunguza mapato ambayo inakubaliwa ). Hata kama hivyo kodi ya mtu binafsi inategemea mabano (bracket) ambayo mtu akomu.

Bonyeza hapa ili upokee cheo cha mapato ya mtu binafsi (for individual)

Kodi ya Shirika/kampuni (Corporation tax)

Ni kodi ambayo inawekwa kwa mtu asiye binafsi/kampuni ambaye anahusika kwa sekta hii kwa cheo cha 30%.

Kodi ya Kuongeza Thamani (VAT)

VAT ni kodi kwa matumizi ambayo  inatozwa kwa cheo cha 18% kwa usambazaji zote ambazo zimefanywa na mtu ambaye anafaa kutozwa kama mtu ambaye amesajiliwa au anayefaa kusajiliwa kwa VAT. Kiwango cha Kusajiliwa kwa VAT cha chini ni mauzo kwa mwaka ambayo inazidi milioni 150 au milioni 37.5 kwa miezi mitatu za kwanza mifulilizo.

Bonyeza hapa kwa habari zaidi za kuhusu VAT

Tafadhali jua:

Watu wote ambao wamesajiliwa kwa VAT wanajukumu wa kusajiliwa kwa EFRIS na kuanza kupeyana ankara (e-invoices) ya kielekroniki.

Bonyeza hapa kwa habari zaidi za kuhusu kusajiliwa kwa EFRIS.

Kodi ya kubakisha (WHT)

  • Kodi ya kubakisha kwa wasambazaii – kama umethibitishwa kukuwa ajenti wa kubakisha kodi, unatarajiwa kubakisha kwa cheo cha 6% kutoka kwa wale waliyo sambaza bidhaa kwako ambayo idadi ya usambazaji inazidi UGX 1,000,000 kwa kila shughuli.
  • Kubakisha kodi kwa malipo kwa mtu aliye burudisha umma asiye mkazi (non resident public entertainer) – kodi hii inatozwa kwa cheo cha 15% kwa jumla ya idadi ya malipo ambayo mtu asiye mkazi ambaye ameburudisha umma. Kodi inabakishwa na kulipwa kabla ya yule aliye burudisha umma kuondoka nchini.
  • Kubakisha kodi kwa malipo kwa wale wa ndani ya nchi waliyo burudisha umma – kodi hii inabakishwa kwa cheo cha 6% kwa jumla ya idadi halafu inawashilishwa kwa URA.

Bonyeza hapa kwa habari zaidi za kuhusu kodi ya kubakisha.

Lipa Ukiingiza Malipo  (PAYE)

Hii ni kodi kwa wahusika ambao wako na wafanyakazi wa (utawala na wa kulipwa kila siku ) ambao wanapokea jumla ya malipo ambayo inazidi Ugx 235,000, aina hii ya kodi inabakishwa kila mwezi.

Bonyeza hapa ili upokee vyeo vya PAYE.

Hizi retani inajazwa  namna ya kujaza retani zingine za mapato.

Bonyeza hapa ili upokee habari zaidi kuhusu urejeshaji wa retani.

Baada ya kurejesha retani unafaa kulipa kodi ambayo inafaa ukitumia jukwaa za malipo ambazo ziko kama benki, pesa kwa simu rununu, EFT, RTGS, VISA, Mastakadi, msimbo (code) wa USSD (*285#) nakadhalika.

Tafadhali jua: tarehe halisi ya kulipa kodi ni sawa na tarehe ya kurejesha retani.

Bonyeza hapa ili usajili malipo

 

Kama hauwezi kujisajili kwa mtandao, tembelea ofisi ya URA iliyokaribu ili upokee usaidizi au piga simu kwa nambari ya bila malipo 0800117000/0800217000 au WhatsApp: 0772140000

 

Print Friendly, PDF & Email
Add to Bookmarks (0)
Skip to content