Biashara ya jumla ni nini?
Biashara ya jumla ni ununuzi wa bidhaa kwa wingi kutoka kwa watengenezaji au wasambazaji na kuziuza kwa muuzaji rejareja kwa kiasi kidogo.
Wauzaji wa jumla wakati mwingine huuza bidhaa kwa watumiaji wa mwisho kwa idadi ndogo.
Biashara ya rejareja ni ununuzi wa bidhaa kutoka kwa wauzaji wa jumla au wasambazaji na kuziuza kwa watumiaji wa mwisho kwa kiasi kidogo.
Katika sekta ya jumla na rejareja, kuna makundi mawili ya walipa kodi.
– Walipa kodi wa Biashara Ndogo wenye mauzo yao kwa jumla hayazidi Ugx 150,000,000
– Walipa kodi waliosajiliwa na VAT na jumla ya mauzo ya kila mwaka zaidi ya Ugx 150,000,000
Biashara zote nchini Uganda zinatakiwa kusajiliwa nazo
Zingatiya yakwamba:
Hautapewa leseni ya biashara isipokuwa uwe na TIN
Bonyeza hapa kwa maelezo kuhusu mahitaji ya usajili wa biashara yako ya jumla/rejareja
Kama mlipa kodi, unastahiki haki. Lakini, kuna majukumu ambayo lazima utimize.
Bonyeza hapa kwa haki na wajibu wako kama mlipa kodi
Unahitaji kuweka rekodi zinazohusiana na miamala yote katika biashara yako. Ni muhimu kila wakati kuwa na rekodi ambazo zina tarehe ili uweze kuelewa ni ripoti zipi zinazohusiana na kipindi gani. Hizi rekodi ni;
Zingatiya ya kuwa Wateja ambao wamesajiliwa kwa VAT lazima watoe ankara za kielektroniki kupitia mfumo wa EFRIS
Bonyeza hapa ili kujifunza zaidi kuhusu EFRIS