VAT ni kodi isiyo ya moja kwa moja (indirect tax) kwa matumizi ambayo inatozwa kwa thamani ambayo imeongezwa kwa bidhaa na huduma kwa hatua nyingi ya uzalishaji na usambazaji. Hapa Uganda VAT inatozwa kwa kila usambazaji ambayo imetekelezwa na mtu ambaye anafaa kutozwa kodi (taxable person) kwa kila uagizaji (imports) wa bidhaa isipokuwa uagizajiĀ (imports) ambazo kodi zimesahemewa (exempt goods) na kwa usambazaji wa huduma isipokuwa huduma ambayo kodi imesamehewa kwa mtu yeyote.
Usambazaji ambayo inatozwa ni usambazaji wa bidhaa na huduma isipokuwa usambazaji ambayo kodi imesamehewaĀ (exempt supply ) ambayo imefanywa Uganda na mtu ambaye anafaa kutozwa kwa thamani (consideration) kama mojawapo wa shughuli la biashara. Usambazaji ambayo inafaa kutozwa inakuwa kwa cheo cha kawaida (standard rate 18%) au cheo cha sifuri (0%), (zero rated).
Kwa mfano usambazaji ambayo inafaa kutozwa VAT.
Hizi ni usambazaji ambayo VAT inatozwa kwa cheo cha 0%. Usambazaji kwa cheo cha sifuri zimeoorodheswa chini cha ratiba ya tatu ya Sheria ya VAT na inajumuisha bidhaa na huduma za kuchukua nje ya nchi, madawa ambazo zimetengenezwa nchini na nafaka (cereals) kama zimepandwa na kushiagwa (milled) Uganda.
Hizi ni usambazaji wa bidhaa na huduma ambayo kodi hazitozwi. Usambazaji ambazo kodi zimesamehewa zimeoorodheshwa kwa ratiba ya pili ya Sheria ya VAT na hizi ni;
JUA: mtu mwenye anafanya shughuli za usambazaji ambazo kodi zimesahemewa (exempt supply) hawafai kusajiliwa kwa VAT na kwa mtu ambaye anafanya shughuli ya biashara ambayo kodi ni kwa cheo cha 0% na kwa usambazaji kwa cheo cha kawaida (standard rate) wanafaa kujisajili kama wamehitimu kwa kusajiliwa.
Hii ni malipo ambayo inaweza kupokelewa kwa pesa au malipo ambayo sio ya kifedha (in kind), zote au nusu kama mtu ambaye amesambaza vitu ambazo zinafaa kutozwa kodi (taxable supply).
Mtu inajumuisha mtu binafsi, ushirikisho (partnership), trusti/uaminifu, kampuni, fedha ya kustaafu (retirement fund), Serikali, chama cha kisiasa madogo madogo ya serikali na mataasisi ambazo zimeoorodheshwa (political subdivisions of the government and listed institutions).
Mtu ambaye anafaa kutozwa:
Kodi ya pembejeo inamaanisha kodi ambayo inalipwa au inalipwa kwa usambazaji/ununuaji wa bidhaa /huduma ambayo inafaa kutozwa au uagizaji (imports) ambayo imefanywa na mtu ambaye anafaa kutozwa kwa mfano yule ambaye anatengeneza maji na amenunua vyombo vya kupakia bidhaaĀ (packaging material ) VAT ambayo mtu anatozwa kwa nyenzo (materials ) ya upakiaji ni pembejeo ya VAT, (INPUT TAX).
Hii ni VAT ambayo inatozwa kwa mtu ambaye anafaa kutozwa kodi kama anauza vitu za kusambazwa ambazo zinafaa kutozwa ushuru. Kama mtu amesajiliwa kwa VAT anafaa kutoza VAT kwa mauzo za vitu ambazo zinafaa kutozwa VAT ambayo inatozwa ushuru ni kodi kwa mauzo (output tax).
Kama kodi ya autiputi ya VAT mtu (VAT kwa mauzo ) inazidi VAT ya pembejeoĀ (VAT kwa ununuaji au gharama), tafauti ni VAT ambayo inafaa kulipwa kwa URA. Kama pembejeo ya VAT (input VAT) ni zaidi ya autiputi ya VAT, tafauti ni VAT ambayo inafaa kudaiwa (VAT claimables) na mtu. Mtu ambaye pembejeoĀ (input ) ni zaidi ya autiputi na kwa hivyo ni VAT ya kudaiwa mtu anaweza kuamua kupokea rifandi kwa URA kama idadi ambayo inafaa kudaiwa ni zaidi ya shilingi milioni 5 au kumaliza deni/ ku-ofseti idadi ya VAT ambayo inadaiwa kwa VAT ambayo itafaa kulipwa mbeleni.
VAT inasanywa kwa kila hatua/steji ya uzalishaji wa bidhaa na huduma. Kama mtu ameagiza (imports) au anatengeneza vifaa wanatozwa VAT kwa vitu ambazo wanatumia kwa kutengeneza vifaa hizo pamoja na gharama ambazo zimetokea. Kama mtu amefanya mauzo kwa mwenye kufanya mauzo ya jumla (wholesaler) wanatoza VAT. Tafauti kati ya VAT ambayo wametoza na VAT ambayo wametozwa ni chenye wanalipa. Hii inaendelea hadi mpaka kama bidhaa zimefika kwa mwenye kutumia bidhaa/huduma wa mwisho (final consumer) ambaye analipa VAT zote, ambayo inamaanisha eti VAT ni kodi kwa mwenye matumizii wa mwisho (final consumer).
Ni mtu ambaye anafanya shughuli ya biashara au anatarajia kufanya biashara anafaa kutuma maombi ya kusajiliwa kwa VAT. Kama mauzo ya bidhaa au huduma kwa miezi mitatu mifulilizo inazidi Shilingi milioni 37.5 au kwa miezi kumi na mbili, jumla ya mauzo kwa mwaka ambayo inafaa kutozwa VAT inazidi Shilingi milioni 150. Usambazaji huu unaweza kukuwa kwa cheo cha kawaidaĀ (standard rate) na cheo cha sifuriĀ (zero rated).
Kusajiliwa kwa VAT inaweza kukuwa ya kujitakia au ya lazima (voluntary or cumpulsory).
1) Kusajiliwa ya lazima
Kama kwa miezi mitatu za kalenda zilizopita mtu amefanya mauzo ambayo thamani yake bila VAT inazidi Shilingi milioni 37.5 mtu huyo anafaa kusajiliwa kwa maramoja VAT. Au kama mtu ana-sababu kama antarajia kwa muda ya miezi mitatu mifulilizo idadi ya thamani kwa jumla la mauzo ambayo inafaa kutozwa inaweza kuzidi shilingi milioni 37.5 kwa haya mtu anahijitajika kujisajili kwa VAT.
2) Kujisajili kwa hiari/kujitakia (voluntary registration)
Mtu ambaye mauzo yake haizidi shilingi milioni 37.5 kwa kila miezi mitatu au milioni 150 kwa miezi 12 anaweza kujisajili kwa hiari yake, mtu kama huyu anafaa kuridhisha URA eti ako na sehemu daima/milele ya kufanyia biashara, anaweza kuweka rekodi vizuri na ni mtu timamu (fit and proper).
Kutoa hesabu ya VAT kama thamani ya usambazaji sio rahisi kugunduliwa.
VAT kwa bidhaa au huduma ambayo thamani yake sio rahisi kutambuliwa, hesabu ya hazina ambayo inaweza kutumika ni thamani ya bei sawa na ile ambayo iko kwa masoko wakati usambazaji umefanywa kama biasharaĀ wa kubadilishana bidhaa/bata ya Ā bidhaa, zawadi, mwenye biashara akitumia bidhaa.
Kama umesajiliwa, mtu anahitajika ku;
EFRIS ni suluhu ya biashara mahiri/erevu (smart business solutions) ambayo biashara inatumia kwa kupeyana risiti ya kielekroniki au ankara ya kielekroniki na kuchunga/kudhibiti namna stoki inapunguka au inaongezekana kwa saa halisi. Walipakodi ambao wamesajiliwa kwa VAT wanafaa kutumia EFRIS ili kutoa ankara ya kielekroniki kwa wateja. Hao pia wanafaa kununua bidhaa au huduma kwa wasambazaji ambao wanapeyana ankara ya kielekroniki kama vifaa ambazo zimenunuliwa ziko na VAT. Hata kama hivyo walipakodi ambao hawajasajiliwa kwa VAT pia wanaweza kutumia EFRIS kwa hiari yao/wakitaka kwa (hali watapeya mteja risiti ya kielekroniki).
VAT inatozwa kwa cheo cha 18% kwa kila hatua/steji ya uzalishaji (production)/usambazaji kwa thamani ambayo imeongezwa kwa bidhaa au huduma ambazo zinafaa kutozwa. Kila mteja ambaye amesajiliwa kwa VAT kwa hatua ya uzalishaji anahaki ya kupewa krediti ya VAT ambayo amelipa zaidi (excess VAT incurred).
Mwenye kutumia bidhaa/huduma ya mwisho (final consumer) mteja ambaye hajasajiliwa kwa VAT hafai kupokea krediti ya kodi na kwa hivyo yeye ndio anapokea uzito wa kodi. Hii inamaanisha eti kodi ambayo inafaa inakreditiwa kwako na kodi ya Serikali inalipwa kwa URA namna imeelezwa chini:
Maelezo Ā |
Bei bila VAT |
Cheo cha kodi Ā |
Idadi ya VAT Ā |
Bei ambayo iko/ imejumuisha VAT Ā |
Ununuaji (purchases)
|
1000
|
18% |
180 |
1180 |
Mauzo (sales) |
1500 |
18% |
270 |
1770 |
Kuhesabu
Kodi ya mauzo/autiputi VAT Ugx 270 ukiondoa pembejeoĀ (input) VAT Ugx 180
Kwa hivyo, Ugx 90 mfanya biashara analipa kwa URA.
Kama mfanya biashara anafanya shughuli kupita kwa EFRIS hesabu ya juu inafanywaĀ kiotomatiki. Kwa wakati wa kurejesha retani ya VAT ya kila mwezi kwa URA, mfanyabiashara ako na jukumu la kuhakikisha na kuweka habari hizi ili ziwe za kisasa kabla ya kutuma kwa URA.