Hapa Uganda, biashara nyingi zinaendeshwa kwa njia isiyo rasmi, biashara kama hizo hazidumu hadi mwaka moja kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi kamilifu ya kusimamia biashara kama hizo. Biashara zingine hazi-heshimu sheria na masharti. Ili iwezeshe ukuaji (growth) wa biashara na kudumu yake. Wenye biashara kama hawa wanafaa kupewa ujuzi (skills) ya kuendesha biashara. Baadhi za ujuzi wa usimamizi wa fedha ambazo wenye biashara wanafaa kukuwa nayo ni kama hizi:
Hii inasaidia kwa kuelewa wateja/soko mahitaji yako na kuchambua (analyse) washindani wako kwenye biashara. Hii inaboresha uamuzi wako kwa soko, huduma na bidhaa. Utafiti (research) kuhusu soko na kwa tasnia (industry) ambayo unawekamu uwekezaji. ili kuzuia, kufanya hasara.
•Tambua wateja, upendeleo na mahitaji yako.
• Gundua mtindo (trends) ambazo ziko kwa soko ili ikuwezeshe kuelewa kama kuna mabadiliko ambazo ziko kwa soko, kama teknolojia na washindani wako.
• Tathmini (assess) na chambua washindani wako kuhusu nguvu na upungufu zao ili utambue nafasi bidhaa/huduma ili uziweke tafauti.
• Tathmini (evaluate) ukubwa wa soko na uwezekano wa kuwezesha biashara kukua ambayo itasaidia kukadiri (estimate) mapato na gharama.
Hii inahusisha kuweka mpangilio wa mahitaji za biashara kama bajeti za gharama na kutambua vyanzo vya mtaji (saurce of capital) kama mkopo, ruzuku (grants) au mwekezaj. Hii inahakikisha eti biashara iko na mtaji ambayo itawezesha uendeshaji wa biashara na kukua kifedha.
• Weka na pia tafautisha mpango wa biashara, mapato ya kibinafsi na gharama.
• Chagua huduma/chanzo cha kifedha cha kutegemewa kwa mfano SACCO, Kampuni ya mkopo mdogo (microfinance) , benki ya kibiashara (commercial bank).
• Weka lengo kwa kile ambacho biashara inahitaji, weka lengo la kifedha na weka juhudi la kutafuta fedha ili kutimiza mahitaji za biashara.
• Weka bajeti ya kulingana na mapato yako ili kuzuia kuingia kwa deni.
• Weka fedha ya uwekezaji ili ;liwezeshe mapato kukua.
• Tafuta usaidizi wa kifedha kama kuna mahitaji kwa kupitia kwa mkopo wa riba la chini na mpangilio rahisi ya kuwezesha urejesheleaji wa fedha rahisi na weka mpango wa kutumia fedha/pesa kwa njia bora.
3.UJUZI WA MAHITAJI YA KISHERIA NA UDHIBITI WA BIASHARA
Tafuta kuelewa sheria na masharti fulani ya kuhusu utawala wa biashara. Kwa kufuatilia mahitaji hizi utazuia biashara yako kupokea tatizo la kisheria, kutunza maendeleo na operesheni nyororo kwa biashara.
• Andikisha jina la biashara na Bodi ya Uganda wa Huduma ya Usajili (URSB) na pokea cheti cha usajili wa biashara au cheti cha usajili wa Kampuni.
• Pokea Nambari ya Kutambua Mlipakodi (TIN) kwa kupitia kwa tovuti ya Shirika ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), au tembelea ofisi ya URA iliyokaribu nawe au piga simu kwa nambari isiyo ya malipo ya 0800117000/0800217000.
• Pokea leseni la biashara kutoka kwa KCCA au kwa Sherikali ya Mtaa, ambayo inakuruhusu kufanya biashara kwa eneo hilo.
• Tafuta Shirika ya Kitaifa cha Udhibiti wa Viwango Uganda (UNBS), Shirika ya Mamlaka ya Dawa (NDA), baadhi za zingine za kutoa ushauri na masharti za kuhusu biashara.
Jua:
Ili usajiliwe kwa kodi unahitaji zifuatazo
(i) Mtu binafsi Kitambulisho cha Kitaifa (ID) au hati yoyote mbili za Kukutambua kama Pasipoti, ID ya kuajiriwa, Leseni la kuendesha gari, ID ya uhamiaji nakadhalika.
Kampuni: Cheti cha Kusajili kampuni, TIN ya Mkurugenzi, Fomu ya 7 ya Kampuni na kadhalika.
Weka rekodi ya biashara sahihi na rekodi ambayo imewekwa vizuri vya shughuli vya biashara zote, Ambazo zinaeleza mapato za biashara ambazo zimepokelewa kwa ununuzi na gharama ambazo zimetokea. Juhudi hizi zitakuwezesha kwa kufuatilia faida ambazo ni muhimu kwa mafanikio na maendeleo ya biashara.
• Omba risiti kutoka kwa msambazaji wa bidhaa wakati wowote ukinunua bidhaa.
• Mpa wateja risiti wakati wowote ukiuuza bidhaa.
• Andika chini gharama ya biashara na weka rekodi ya kuhusu wafanyakazi.
• Weka rekodi zote za kuhusu kodi ambayo inaeleza malipo uliyofanya kwa URA (kodi).
Vitu ambazo unafaa kuelewa ya kuhusu kuweka rekodi
a) Kuweka rekodi ni muhimu sana kwa biashara kwa lugha la Kingereza kama unataka kuweka rekodi kwa lugha tafauti au sarafu (currency) utatuma maombi kwa maandiko na sababu kwa Kamishna ili upokee ruhusa.
Jua:
Kama rekodi inahitajika kwa kesi ambayo ilianza kabla ya miaka tano kukamilika. Mlipakodi ataweka rekodi hadi kesi kukamilika
b) Weka rekodi kwa miaka mitano baada ya mwaka wa fedha kukamilika litasaidia kwa kumbukumbu (reference).
c) Rekodi ambayo imewekwa inafaa kukuwa na habari kamilifu na kuwekwa kwa fomati ambayo inaweza kubadilishwa kwa fomati ya kawaida (standard format) ambayo inaeleweka kwa urahisi.
d) Tuma maombi kwa maandiko ikikuwa na sababu sahihiI kwa Kamishna ili upokee ruhusa kama unataka kuweka rekodi kwa lugha tafauti au sarafu (currency).
Jua:
Idadi ya rekodi ambayo inawekwa italingana na ukubwa wa biashara. Biashara ambayo iko na mauzo kwa jumla la milioni 500 kwa mwaka lazima kitabu cha kuhesabu hazina liwekwe (audited books of accounts).
Elewa wajibu wako wa kodi na weka harakati ya kupunguza gharama ya kodi. Hii inaweka msingi kwa biashara ya kujulisha au kujua wakati wa kulipa kodi. Ambayo inarahisisha ufuatiliaji wa sheria za kodi.
Manufaa za kupokea kama umepata TIN
TIN itakuwezesha;
Namna ya kupokea TIN
TIN ya kupokea kwa haraka (instant) ya mtu wa kibinafsi
Hatua ya 1. Tembelea tovuti ya URA kwa https://ura.go.ug na kwa peji ya nyumbani ya URA. bonyeza ” Get a TIN”
Hatua ya 2. Bonyeza “Instant TIN application”
Hatua ya 3. Kwa upokeaji wa TIN wa haraka (instant) bonyeza kutuma maombi ya kupokea TIN kwa haraka.
Hatua ya 4. Kwa peji ya nyumbani ya usajili wa TIN cha mtu binafsi kama kategoria ya kutuma maombi.
Hatua ya 5: Weka nambari ya ID ya Kitaifa (NIN) chanzo cha kodi na sehemu ya kisasa ambayo unafanyia biashara. Boxi ambayo iko na nyota nyekundu ni ya kujazwa kwa lazima.
Hatua ya 6: Bonyeza tuma maombi, baada ya kuthibitisha eti wewe sio roboti.
Jua:
Kama chanzo cha mapato ni ya kutoka kwa kuajiriwa, TIN ya muajiri ni lazima kwa biashara ambayo imesajiliwa. Tarehe ya kusajili biashara, jina na nambari ni ya lazima. Baada ya kutuma maombi utapokea TIN kwa haraka “instant” na cheti cha TIN cha muda (provisional) utapokea.
|
Aina ya retani |
Tarehe sahihi ya malipo ya kodi na maelezo kuhusu retani |
|
Kodi ya mapato |
• Unahitajika kurejesha retani ya kodi ya kukadiria ya muda (estimate of provisional tax) |
|
• Unahitajika kurejesha retani ya kodi ya mapato ya mwisho ikijumuisha kodi ya ukodishaji (rental tax), kama ukonayo kwa kila mwaka wa fedha kabla ya miezi sita baada ya mwaka wa fedha kukamilika. |
|
|
VAT
|
•Kama imesajiliwa kwa Kodi ya Kuongeza Thamani (VAT). Unahitajika kurejesha retani ya kila mwezi kwa tarehe 15 ya mwezi ujao. |
|
PAYE |
• Kama umesajiliwa kwa kodi ya (PAYE) unahitajika kurejesha retani ya (PAYE ) ya kila mwezi kwa tarehe 15 ya mwezi ujao |
|
Kodi ya madhara (Excise duty) |
• Kama umesajiliwa kwa kodi ya madhara “Excise duty” unahitajika kurejesha retani kwa tarehe 15 ya kila mwezi ujao.
|
|
Kodi ya kubakisha (WHT) |
• Kama umechaguliwa na Serikali ili ubakishe kodi (WHT). Kama unanunua mali ya biashara (business asset) au kufanya malipo ya nauli ya huduma ya kitaaluma (professional service). Unahitajika kurejesha retani ya WHT ya kila mwezi kwa tarehe 15 ya mwezi ujao. |
|
Zingine |
• Kama retani zingine zinahitajika kurejeshwa chini cha sheria ya kodi. Zinahitajika kufanywa kwa muda fulani chini cha sheria ya kodi.
|
|
|
|
Jua:
a) Retani zote za kodi lazima zirejeshwe kwa fomati ambazo zimethibitishwa, na Kamishna na pia anaweza kuchagua mtu ili asaidie mlipakodi ambaye hawezi timiza shughuli ya kurejesha retani hii itafanywa kwa gharama ya mlipakodi.
Kodi inalipwa kutoka kwa wakati wa kusajili malipo kimtandao kwa tovuti ya URA au kwa kutumia “ASK URA APP” shukisha (download) kutoka kwa “Google store” au bonyeza*285# ili uweke malipo au unaweza kuweka kwa benki, pesa kwa simu rununu (mobile money), au kwa huduma ya “payway”.
Hatua za Kusajili malipo
Hatua ya 1.Tembelea tovuti ya URA kwa https://ura.go.ug na kwa peji ya nyumbani bonyeza weka malipo “make payment”.
Hatua ya 2. Kwa orodha (menu) kwa sehemu ya mkono wa kushoto kwenye kompyuta. Bonyeza karatasi “payslip” ya kufanyia malipo na chagua bonyeza hapa ili usajili malipo “click here to make payment”.
Hatua ya 3: Kwa peji ya kusajili malipo
• Chini cha habari ya kuhusu mlipakodi kwa kina, weka TIN ya mlipakodi, jina la mlipakodi, wilaya/mji mkuu.
• Chini cha muda, chagua muda ya kodi ambayo unaweka malipo.
• Chini cha chanzo cha malipo, chagua aina ya malipo unayotaka.
Hatua ya 4: Chini cha chanzo cha malipo>>Kichwa cha kodi, chagua kichwa cha kodi kanuni, ambayo unataka kufanyia malipo kwa mfano kodi ya mapato, na bonyeza kwa muda ambayo unataka kufanyia malipo.
Hatua ya 5: Chini cha muda ambayo unataka kufanyia malipo (load period), jazaa muda ambayo unafanyia malipo halafu bonyeza ongeza muda.
Hatua ya 6: Ifuatayo jazaa idadi pesa ya kulipa.
Hatua ya 7: Chini cha aina ya malipo, weka neno kutoka kwa picha (words from the image) ambayo umepewa na bonyeza eti umekubali halafu jisajili.
Hatua ya 8: Kama umesaa sukuma, karatasi ya kusajili malipo (payment slip) itatengenezwa. Elewa nambari ya karatasi ya usajili/kufanyia malipo ambayo imewekwa kwa karatasi ya usajili wa malipo (payslip) chapisha karatasi ya malipo halafu weka malipo kwa benki au kwa kupitia kwa pesa kwa simu rununu, au aina zote za malipo ambazo zinakubaliwa na URA.
JUA:
• URA au afisa wa URA yeyote hawapokee pesa taslimu (they don’t receive cash payments).
• Hakikisha eti unabakisha kodi (WHT) ambazo zinahusiana, kama PAYE kabla ya kufanya malipo.
• Fanya ukadiri wa (estimate) malipo ya kodi kutoka kwa mwanzo wa mwaka kulingana na jumla la malipo kutoka kwa mwaka uliopita.
• Tembelea ofisi yoyote ya kodi iliyokaribu nawe ukikuwa na swali lolote au ukitaka usaidizi.
(Commissioner of Customs).
Bidhaa hadi za thamani za dola 2000 kama zimeagizwa na mtu/msafiri ambaye amekua nje ya Uganda kwa muda inayozidi masaa (24) mizigo itakubaliwa/ruhusiwa (kusahemewa kodi) bora mizigo msafiri amekuja na mizigo hizo na ametoa tamko (declaration) kwa forodha (customs). Mizigo hizo sio za kugawa kwa marafiki, mandugu, au kwa madhumuni (for business purposes) ya kibiashara isipokuwa kwa matumizi za kibinafsi.
Jua: Hapa kufanya kliarensi kupitia kwa ajenti sio lazima isipokuwa matumizi ya rijimi ya kliarensi ambayo imerahisishwa (simplified clearance regime) PB4 ambayo imesajiliwa na afisa wa forodha (customs). Kama bidhaa zimeletwa kwa sehemu ya forodha kwa mfano sehemu ya mpaka ya kutumia kwa kuingia nchini. Afisa wa forodha lazima wafahamishwe kuhusu mtu ambaye anawajibu wa kulipa kodi mhusika/mwenye bidhaa ambazo ziko kwa chombo/gari/ndege. Hii inaweza kukuwa mwenye bidhaa au ajenti ikijumuisha dalali (broker) wa forodha (customs) au mwenye chombo cha kusafirisha bidhaa mwenye ametoa tamko (declarant).
Kliarensi za bidhaa
Tafauti na mizigo za abiria ambazo zimeelezwa juu hapo. Kama unafanya kliarensi za bidhaa kwa URA (customs) unahitajika kutumia huduma ya ajenti wa forodha ambaye atafanya shughuli kwa niaba yako. Ajenti wa kliarensi wanahitajika kutoa huduma ya kitaaluma kwa niaba ya muagizaji au msafirishaji wa bidhaa nje ya nchi (exporter) . Kila mwaka Kamishna wa forodha hupea ajenti wa forodha leseni la kuwaruhusu kufanya shughuli kwa niaba ya wanabiashara orodha (menu) hii iko kwa tovuti ya URA kwa www.ura.go.ug.
Kila bidhaa ambazo zinaletwa Uganda lazima tamko litolewe kwa forodha, isipokuwa bidhaa zingine kama maiti ambayo ikiletwa Uganda inaweza kuachiliwa bila kuwekwa kwa entri/tamko.
Wewe ama ajenti wako ambaye amethibitishwa munafaa kuweka tamko (declaration) kwa Bili Moja ya Forodha (Customs Single Bill of Entry) au Hati Moja ya Utawala (Single Administrative Document SAD).
Namna ya Kuhesabu kodi wakati wa kuleta bidhaa Uganda
Kuamua Kodi ya kulipa wakati wa kuleta bidhaa Uganda inafanywa kwa kuzingatia thamani ya forodha (customs valuation) cheo cha forodha wa msingi wa “customs tariff nomenclature” (EAC – CET), chanzo cha bidhaa (origin of goods), au vifaa vingine vya kisheria. Ambazo zimeelezwa kwa ratiba zingine za Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (2004).
Jua: Mtu yeyote ambaye hafuatilii sheria ni hatia/makosa na atapewa faini/adhabu au kufungwa itategemea na hatia/makosa ambayo amefanywa.
Thamani ya Forodha
Forodha (customs) itaamua thamani ya bidhaa ili iweze kusanya kodi fulani (specific tax) au kodi ya advalorem (advalorem tax).
Thamani ya Forodha (Customs value)
Kwa bidhaa ambazo zimeletwa nchini kwa kupitia kwa njia/barabara, reli au kwa maji. Thamani ya forodha inajumuisha bei ya bidhaa, gharama ya bima, na rehani “freght” (CIF) na mabadiliko zingine ambazo zimefanywa. Kwa zile ambazo zimeletwa nchini kwa anga (air transport). Thamani ya forodha inajumuisha bei ya bidhaa na gharama ya bima (C&I).
Kwa Kuhesabu kodi kwa madhumuni ya forodha (customs purposes). Aina sita za kuhesabu kodi zitatumika. Aina ya msingi ni aina ya thamani ya shughuli (transaction value method) ambayo ni bei yenyewe ambayo imelipwa au inafaa kulipwa kwa bidhaa. Hata hivyo masharti zifuatazo lazima zitimizwe (fulfilled) ili aina hii itumike. Kama thamani ya shughuli (transaction value) haiwezi kutumika moja kati ya aina zingine zinaweza kutumika ili kuamua thamani ya forodha kwa njia moja ikifuatiliwa na ingine aina hizi ni: aina za thamani za bidhaa ambazo zinafanana kipacha (identical goods value), aina za bidhaa ambazo zinafanana, aina ya kupunguza thamani, aina ya kujumuisha thamani thamani au
aina ya “fallback”.Malipo ya kodi ya forodha
Baada ya tamko kutolewa na ajenti ya kliarensi au afisa wa forodha rijimi ambayo imerahisishwa (simplified regime). Kuthatmini (assessment) inafanywa na kupewa kwa mteja ili alipe kodi ambayo inafaa.
Weka pesa yako pahali ambapo itakuwezesha kupata faida. Unaweza kufanya hizi kwa njia ya kununua mali (property), wanyama, biashara, na kwa shughuli zingine ambazo zitakusaidia kwa kupokea faida.
• Weka lengo na mpango wa uwekezaji bora.
• Fanya uwekezaji mbalimbali ili upunguze hatari/kufanya hasara.
Tahadhari
Habari hii ni ya kipekee cha kutoa ushauri kwa wateja wetu na inaweza kufanyiwa marekebisho ya kisheria, masharti, na kanuni ya kuhusu utawala wa kodi.
Kwa habari zaidi wasiliana na URA kwa:
Kituo kikuu: Ploti M 193/M194 Nakawa, Eneo la Viwanda, S. L. P 7279, Kampala-Uganda, Nambari ya simu 0800117000 | 0800217000, WhatsApp: 0772140000, Emeli:service@ura.go.ug, tovuti: www.ura.go.ug, Facebook:@URApage, Twitter:@URAuganda.