Vifaa Vya Burudani

Vifaa vya Burudani ni nini?

Ni mali ambayo isiyohamashika kwa mfano nyumba au kiwanja cha kutumika kwa burudani ya kibinafsi

na ya jamii, kufurahi au shughuli za kijamii na mahitaji zote za kiraha.
Vifaa vya burudani (recreational) zinaweza kukuwa za ndani ya nyumba au za nje sehemu za kijani kama uwanja wa gofu,

 sehemu ya kufanyia raha, ukumbi wa mazoezi (Gymnasiums), Sinema, mahali ya masaji, mahali pa kambi (camp site) baadhi za zingine.

Add to Bookmarks
Please login to bookmark Close

Biashara zote hapa Uganda zinafaa kusajiliwa na:

  • Ofisi ya Huduma ya Usajili Uganda (URSB) Kusajili Kampuni
  • Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) kwa kodi
  • Mamlaka ya Halmashauri ya Mtaa kama KCCA, Halmashauri ya manispaa, kwa leseni la biashara

Tafadhali jua:
Baada ya kusajili, biashara kwa sekta hii unahitajika kutii masharti ambazo zinahitajika

kutoka kwa mamlaka zinazohusika kama:

  • Bodi ya Utalii wa Uganda
  • Mamlaka ya Kitaifa cha Kudhibiti Mazingira

Kwa mtu wa kibinafsi (Individual)

  • Kitambulisho cha Kitaifa (ID)
  • Cheti cha Usajili/kujisajili

Kwa mtu asiye wa kibinafsi (Non individual)

  • Fomu 20 ya Kampuni
  • Cheti cha kusajili Kampuni

Bonyeza hapa ili upokee mahitaji zaidi za kusajiliwa

Unahitajika kutembelea tovuti ya URA kwa www.ura.go.ug

–  Bonyeza hapa ili ujisajili kama mtu binafsi (for individual)

– Bonyeza hapa ili ujisajili kama mtu asiye wa kibinafsi (non individual)

Kama mlipakodi unahaki  na pia unawajibu ambazo unafaa kutimiza/kufanya.

Bonyeza hapa ili upokee haki na wajibu wako kama mlipakodi.

Aina za rekodi gani ambazo zinafaa/zinahitajika kuwekwa kwa madhumuni (purposes) ya kodi?

Ni muhimu kuweka rekodi zote za biashara vizuri kwa muda isio chini cha miaka mitano baada ya mwaka wa fedha

kukamilika ambazo rekodi zinahusiana nazo.

Na hizi ni

– Taarifa/habari ya Mapato (orodha ya risiti na malipo)

– Mizania ya taarifa ya mapato (balance sheet)

– Orodha ya malipo ya mshahara

– Ratiba ya Uagizaji (import schedule)

– Mikataba/makubaliano

– Habari/taarifa za benki

– Barua za Uajiri

– Bili (za matumizi kama ya maji, umeme)

– Rekodi ya stoki/bidhaa

– Rejista za mali na za rekodi zingine/hati  ambazo zinahusiana na biashara kama kitabu cha risiti, Ankara (invoice), wanao dai biashara na wenye biashara inawadai (debtors and creditors)

Bonyeza hapa ili upokee habari zaidi za kuhusu mahitaji za kuweka rekodi za biashara.

Kodi ya Kuongeza Thamani (VAT)

Kwa mtu ambaye anapokea mapato kutoka kwa vifaa  vya burudani ambazo zinazidi shilingi milioni 150,000,000 kwa mwaka

 fulani, anafaa kusanya VAT kwa kila shughuli ambayo ankara (invoice) imepeyana ya (EFRIS).

Bonyeza hapa ili Usajiliwe kwa VAT

Kodi ya mapato
Mtu yeyote ambayo anafanya shughuli/ biashara ya burudani anahitajika kusajiliwa kwa kodi ya mapato.

 Kodi ya mapato inahitajika kulipwa na mtu yeyote ambaye anapokea mapato yoyote bora ikikuwa mtu binafsi,

mtu asiye wa binafsi au Ushirikiano.

Mtu mkazi (resident person) anahitajika kutozwa kodi kutoka kwa mapato zote ambazo zimepokelewa duniani kote.

Mtu asiye wa binafsi anatozwa kwa malipo ambayo imepokelewa kutoka kwa chanzo cha Uganda pekee.

Kodi ya Kubakisha (WHT)

Kodi ya Kubakisha (WHT) kwa usambazaji wa biashara ya burudani Uganda. Kodi hii inabakishwa kwa cheo cha 6% kwa jumla la idadi kama linazidi

shilingi milioni 1,000,000 na kuwashilishwa/kuperekwa kwa URA.

Retani hizi zina-rejeshwa kama za Kodi za mapato za biashara zingine.

Bonyeza hapa ili upokee habari zaidi za kuhusu urejeshaji wa retani

Baada ya kurejesha retani unahitajika kulipa kodi ambayo inahitajika/inafaa ukitumia Jukwaa za malipo kama benki, EFT, RTGS, VISA, Mastakadi, USSD “code” (*285#) nakadhalika.

Tafadhali jua: tarehe halisi ya kulipa kodi ni sawa na tarehe ya kurejesha retani.
Kama unataka usaidizi zaidi, tembelea ofisi ya URA iliyo karibu nawe au piga simu kwa nambari isiyo ya malipo 0800117000/0800217000 au WhatsApp: 0772140000

Add to Bookmarks (0)
Please login to bookmark Close
Skip to content