Hatua 1- Usafirishaji wa bidhaa
- Mwenye meli ya usafirishaji anapeyana “masta bill” kwa konsolideta
- Konsolideta, anagawa bidhaa kwa Bili ya Nyumba ya kibinafsi (individual House Bill).
- Mwagizaji (importer) anapokea bili ya Nyumba ya kibinafsi (individual House Bill) kutoka kwa kosolideta.
Hatua 2- Kliarensi kwa bandari (Mombasa au Dar es Salaam)
- Konsolideta anachagua ajenti wa forodha (customs) ambaye analeseni ya kufanya kliarensi ili asukume tamko (declarations) la forodha (customs) (WT8) kwa URA.
- Kama imepitishwa na URA, bidhaa inaachiliwa kutoka kwa bandari ili kusafirishwa hadi kwa ghala ya bondi ya forodha Uganda (customs Bonded Warehouse).
Hatua 3 – Kama bidhaa imefikishwa Uganda, inakaguliwa
- Bidhaa ambazo zimeagizwa zinapokelewa kwa pamoja na mlinzi wa ghala (warehouse keeper) na afisa wa forodha (customs) ya URA.
- Kila mwagizaji (importer) anachagua ajenti wa kliarensi ili afanye shughuli ya kliarensi ya bidhaa fulani akitumia bili ya Nyumba ya binafsi (individual House bill) bili ambayo imetafautishwa.
- URA inafanya ukaguzi wa bidhaa zote kimwili cha pamoja kama mwagizaji ako karibu au ajenti wake ili waidhinishe eti tamko (declarations) za bidhaa zote ni halisi.
Hatua 4 – Kufanya Mabadiliko ya umiliki na Kupeyana Bili ya Nyumba (House Bill).
- Konsolideta anatuma maombi kwa URA kwa mfumo wa ASYCUDA ili ubadilishaji wa umiliki ufanyiliwe kwa kila mwagizaji wa bidhaa kwa TIN yake, na kuambatisha Bili ya Ladingi ya Nyumba ambayo inahusiana (House Bill of Lading).
- URA inapitisha na kuweka rekodi ili liwe la kisasa likihusiana na mwenye bidhaa halisi.
Hatua 5 – Ulipaji wa kodi na Mwagizaji
- Ajenti wa mwagizaji ambaye amechaguliwa anachagua tamko (declaration) la utumishi wa nyumbani (declaration for home use) (IM4) na halafu analipa kodi halisi ya bidhaa.
- URA inaidhinisha na kuthibitisha malipo.
Hatua 6 – Kutoa bidhaa
- URA inaachilia bidhaa ya mwagizaji kama utaratibu zote zimekamilka.
BIDHAA YAKO, NI KIPAUMBELE CHETUS!