Muhtasari ya sekta ya Uvuvi

Uvuvi ni nini?

Uvuvi ni shughuli ya kukamata samaki kutoka kwa chanzo cha maji, kwa matumizi ya nyumbani au ya kibiashara.

Uvuvi ni shughuli ambayo sana sana inafanywa kwa maji safi Uganda ikijuimuisha ziwa na mto. Samaki zingine zinapatikana kwa wakulima ambao wanazitunza kwa bwawa za samaki (fish pond).

Kategoria ya wahusika wengine kwa sekta hii ni wale ambao wanafanya shughuli ya usindikiaji wa samaki ya kuongeza thamani kwa samaki ya kusafirishwa nje (export).

 

 

 

Add to Bookmarks
Print Friendly, PDF & Email
(Visited 71 times, 1 visits today)

Mvuvi ni mtu wa kuvua samaki ya kuliwa au ya kuuza.

Mchuuzi wa samaki ni mtu wa kuuza samaki kwa mtu wa kufanyisha ya mwisho (final consumer).  Mchuuzi wa samaki  anaweza kukuwa mtu wa kuuza kwa jumla au wa kuuza kwa riteli (moja moja) ambaye ako na uzoefu (experience) kwa kuchagua, kununua, kutunza, kuchoma samaki,” boning”, kufanya maonyesho na kuuza bidhaa za samaki.

Wahusika wote ambao wako kwa sekta la uvuvi Uganda wanahitajika   kusajiliwa na;

– Ofisi ya Huduma ya Usajili Uganda (URSB) kwa kampuni au jina la biashara

– Shirika ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) kwa kodi.

Tafadhali jua:

Kama umesajiliwa, unafaa kufuatilia masharti za mashirika za kisheria kama;

  • Shirika la Kitaifa cha Usimamizi wa Mazingira (NEMA).
  • Idara ya Kudhibiti Uvuvi, Masharti na Kuhakikisha Kiwango kizuri chini cha Wizara wa Kilimo, Viwanda vya Wanyama na Uvuvi.
  • Kwa wavuvi na wachuuzi leseni lako haliwezi kurudishwa upya (renewed) hadi mpaka ukiwa na TIN.

Kwa mtu binafsi (For individual )

– Kitambulisho I’D

– Cheti cha Kusajiliwa

Kwa mtu asiye binafsi (For non individual)

– Fomu ya Kampuni 20

– Cheti cha Kusajili kampuni (Certificate of incorporation)

Bonyeza hapa ili upokee habari kwa kina kuhusu usajili wa biashara ya Uvuvi.

Unahitajika kutembelea tovuti ya URA ya www.ura.go.ug

Bonyeza hapa ili usajiliwe kama mtu binafsi (for individual)

Bonyeza hapa ili usajiliwe kama mtu asiye binafsi/kampuni (for non individual)

Bonyeza hapa ili upokee haki na wajibu wako kama mlipakodi

Unafaa kuweka rekodi ambazo zinahusiana na shughuli za biashara zako. Ni muhimu kukuwa na rekodi ambazo ziko na tarehe hii itakuwezesha kujua muda wa ripoti au wakati wa ripoti na hizi ni;

  • Rekodi ya taarifa ya mapato
  • Rekodi ya risiti /Ankara (invoices)
  • Mizania (balance sheet)
  • Orodha ya malipo ya wanyakazi (payroll) na mkataba/barua ya kazi
  • Ratiba ya uagizaji (import schedules) kama iko
  • Taarifa/habari ya benki
  • Bili ya Matumizi kama ya (umeme au maji)
  • Rekodi ya stoki ya samaki
  • Rejesta ya mali (Asset register)
  • Watu wanaodai biashara na wenye biashara inawadai (debtors and creditors).
  • Mkataba wa usambazaji na malipo (contracts of supply)
  • Ratiba ya uagiza wa bidhaa na huduma (import schedules)

Weka rekodi vizuri vya shughuli za biashara zote kwa lugha ya kingereza.

–  Kama unataka kuweka rekodi kwa lugha tafauti, sarafu, tuma maombi kwa maandiko ukiweka sababu sahihi kwa Kamishna ukiomba ruhusa.

– Kama rekodi haijawekwa kwa lugha ya kingereza, utahitajika kugharamia kutafsiriwa (translations) kwa lugha ya kingereza na mtafsiri  ambaye amethibitishwa na Kamishna.

– Weka rekodi ili irahisishe uamuaji wa kodi wako;

– Weka rekodi kwa miaka mitano baada ya muda wa kodi kukamilika ambayo inahusika ili mbeleni kama kuna mahitaji ya kukagua vitabu au hati itakuwa rahisi

– Kama rekodi inahitajika kwa shughuli ambayo ilianza kabla ya miaka mitano kukamilika , utahitajika kuweka rekodi mpaka shughuli kukamilika

– Rekodi ambayo imewekwa inafaa kukuwa na ushahidi ambayo inatosha za taarifa/ habari za biashara na inafaa kuwekwa kwa umbizo/fomati ambayo itakuwa rahisi kubadilishwa kwa namna ya kawaida (standard form) ambayo itakuwa rahisi kueleweka.

 

 

Maelezo

Motisha ya kodi

Malori za friji

Kusahemewa kodi zote chini cha ratiba ya 5 ya Shirika ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2004.

Nyumba baridi

Nyumba baridi ambayo ina halijoto ambayo mazingira yake inadhibitiwa kama ya friji

Kodi ya uagizaji ni 0% kulingana na EAC CET inasadia kwa kudhibiti mavuno na uwekaji wa bidhaa za kilimo kwa nyumba baridi kama nyama ya ngombe, nyama ya kuku na samaki nakadhalika

 

 

Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea ofisi ya URA ili upokee usaidizi au piga simu kwa nambari ya bila malipo ya 0800117000/0800217000 au WhatsApp: 0772140000

 

Print Friendly, PDF & Email
Add to Bookmarks (0)
Skip to content