Sekta ya Burudani

Burudani ni nini?

Burudani ni shughuli ambayo inavutia umakini na nia ya watazamaji au inaleta raha. Burudani ya umma inajumuisha shughuli kama tamasha (concert) na utendaji (performance).

Add to Bookmarks
Print Friendly, PDF & Email
(Visited 14 times, 1 visits today)

Wahusika muhimu kwa kiwanda hiki ni:

Promota/meneja wa tukio, VJs, DJs, MCs, wenye kuandika nyimbo, shairi, wana-muziki, wenye kuigiza filamu, wenye kufanya kama mifano (models), na watayarishaji wa muziki au tukio (producers) nakadhalika.

Watu wote ambao wanapokea mapato kutoka kwa biashara ya burudani. Wanajibika kusajiliwa na URA kwa kodi. Kila wahusika kwa sekta ya burudani Uganda wanafaa kufanya biashara liwe rasmi kupita kwa mashirika zifuatazo.

– Wizara wa Jinsia Kazi na Maendeleo ya Kuboresha maisha ya Jamii.

– Shirika ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) kwa kodi na kupokea TIN

– Kukuwa mwana chama kwa chama ambacho umechagua ili kuyungana nacho kama Muungano ya Wanamuziki wa Uganda, Muungano ya Promota/watangazaji Uganda nakadhalika

– Kwa mtu asiye binafsi/kampuni unaweza kusajili taasisi yako na Ofisi ya Huduma ya Usajili Uganda  (URSB)

Kwa mtu binafsi (for individual)?

– Kitambulisho I’D

– Cheti cha Kusajiliwa

Bonyeza hapa ili upokee habari kwa kina kuhusu kusajiliwa

Unafaa kutembelea tovuti ya URA kwa www.ura.go.ug

Bonyeza hapa ili ujisajili kama mtu binafsi (for individual)

Bonyeza hapa ili ujisajili kama mtu asiye binafsi/kampuni (for non individual)

Bonyeza hapa ili upokee habari za kuhusu haki na wajibu wako kama mlipakodi

Ni muhimu kuweka rekodi ya shughuli ya biashara zote vizuri kwa miaka kisicho chini cha tano baada ya muda ya kodi kukamilika ambazo zinahusiana nazo kwa kumbukumbu mbeleni.

Hizi ni;

– Taarifa ya mapato  (orodha ya risiti na malipo)

– Mizania (balance sheet)

– Ratiba ya malipo ya mshahara (payroll)

– Ratiba ya uagizaji  (import schedules)

– Mkataba

– Barua ya kuajiriwa

– Taarifa ya benki

– Bili kwa mfano bili ya matumizi kama ya maji au umeme

– Rekodi ya bidhaa/stoki

Rejesta ya mali na rekodi zingine mengi na/au rekodi ambazo zinahusiana na biashara kama kitabu cha risiti, ankara (invoices) wanaodai na wenye biashara inawadai (creditors and debtors).

Bonyeza hapa ili upokee habari zaidi ambazo zinahusika na kuweka rekodi za biashara.

Kodi ya kubakisha (WHT):

  • Kubakisha kodi kwa malipo kwa mtu asiye mkazi ambaye anaburudisha umma. Kodi hii inatozwa kwa cheo cha 15% kwa jumla ya malipo ambayo imepokelewa na mtu asiye mkazi (non residents) ambaye anaburudisha umma. Kodi inabakishwa na kulipwa kabla ya mtu asiye mkazi aliyefanya burudani kwa umma kuondoka nchini na itakuwa kodi ya mwisho.
  • Kubakisha kodi kwa malipo kwa msambazaji kwa sekta ya burudani. Kodi hii inabakishwa kwa cheo cha 6% kwa jumla ya idadi kama inazidi UGX 1,000,000 na kuwashilishwa kwa URA.

Kodi ya Kuongeza Thamani (VAT)

Kwa wahusika ambao wanazalisha mapato kutoka kwa sekta ya burudani ambayo inazidi UGX 150,000,000 kwa mwaka fulani, wanafaa kusanya VAT kwa kila shughuli ambayo ankara (invoice) imepewa (EFRIS)

Tafadhali jua:

Tiketi zote ambazo zimetolewa kwa wanao-hudhuria burudani inavutia kodi kwa cheo cha 18% (ikijumiisha VAT).

 

Hizi retani zinajazwa namna ya kujaza retani zingine za kodi za mapato

Bonyeza hapa ili upokee habari kuhusu namna ya kurejesha retani.

Baada ya kurejesha retani unafafaa kulipa kodi ambayo inafaa kwa kutumia jukwaa kama benki, simu rununu, VISA, Mastakadi nakadhalika.

Tafadhali jua:

Tarehe halisi ya kulipa kodi ni sawa na tarehe ya kurejesha retani.

Kama unataka usaidizi zaidi, tembelea ofisi ya URA au piga simu kwa nambari ya bila malipo ya 0800117000/0800217000 au WhatsApp: 0772140000

 

 

 

 

 

 

 

Print Friendly, PDF & Email
Add to Bookmarks (0)
Skip to content